Kwa picha: watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Adhuhuri wa Ijumaa tarehe (7 Dhulhijja 1440h) sawa na (9 Agost 2019m) yamefanyika matembezi ya pamoja kati ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu wa tano Muhammad Albaaqir (a.s).

Matembezi yalianzia ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumpa pole waombolezaji wakaelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu huku wakiimba kaswida zinazo amsha hisia za huzuni kutokana na msiba huu mkubwa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s), walipo wasili katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) wakapokelewa na ndugu zao watumishi wa bwana wa watu huru na kuomboleza kwa pamoja, wakafanya majlis jirani na kaburi la Abu Abdillahi Hussein (a.s) na mazuwaru waliokuwepo hapo wakashiriki kwenye majlis hiyo.

Fahamu kua leo ni mwezi saba Dhulhijja, tarehe kama ya leo ulifariki Imamu wa tano Muhammad bun Ali Albaaqir (a.s) ni msiba unao umiza sana nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s), siku hii huombolezwa dunia nzima, mapema leo asubuhi mawakibu za waombolezaji zilianza kumiminika katika mji wa Karbala kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na Imamu wa zama (a.f) kutokana na msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: