Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, chini ya usimamizi wa makamo katibu mkuu wa Ataba na mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi, msafara wa kutoa misaada (washirika wa ushindi) umeondeka kuelekea Samaraa asubuhi ya Ijumaa (7 Dulhijja 1440h) sawa na (9 Agost 2019m) kutoa misaada ya kibinadamu kwa familia za watu wenye kipato cha chini na familia za wakimbizi,msafara huo umeongozwa na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na mawakibu zaidi ya (250) zinazo fungamana nayo, misaada wanayo toa ni vifaa vya nyumbani, hela na chakula, vitu hivyo vimetolewa na mawakibu hizo kutoka mikoa tofauti ya Iraq, wanatarajia kusaidia zaidi ya familia (2500) katika mji huo (Samaraa).
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Shekh Maitham Zaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Leo tumekuja katika mji huu kipenzi kuwasaidia ndugu zetu wa Samaraa, kama mnavyo fahamu tupo karibu na Iddi tukufu, kwa hiyo tumegawa nguo za Iddi kwa watu masikini na familia za mashahidi”.
Akaongeza kua: “Sisi tunatekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu kutoka Najafu, tulipo kwenda kumtembelea na kumpokenza kutokana na ushindi, alisema: Ushindi ni wa raia wa Iraq, hakika adui aliyekuja Iraq alikua wa kimataifa, hakuilenga Iraq peke yake bali nchi zote, raia wa Iraq wakasimama imara kupambana na adui huyo. Na usia wake mkubwa kwa raia wa Iraq alisema: Saidieni familia za mashahidi, saidieni familia na masikini, msafara huu ni kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani”.
Naye kaimu kiongozi wa Maqaam Samaraa Ustadh Mahmuud Khalf Ahmad akasema kua: “Kutoka katika mimbari hii natoa shukrani nyingi kwa wakili wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na kila aliye changia misaada hii, tunaomba kuendeleza jambo hili linalo toa ujumbe wa wazi kua raia wa Iraq ni wamoja kuanzia kaskazini hadi kusini”.