Kutokana na kumbukumbu ya kifo cha balozi wa Imamu Hussein na mtoto wa Ammi yake Muslim bun Aqiil (a.s) na katika ratiba yake maalum ya kuomboleza msiba huu, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Jumamosi (8 Dhulhijja 1440h) sawa na (10 Agost 2019m) umefanya majlis maalum kwa watumishi wake katika ya ukumbi wa utawala ndani ya Ataba tukufu.
Majlis ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha Shekh Muhsin Khaqaani kutoka kwenye kitengo cha dini akatoa mawaidha, akamzungumzia Muslim bun Aqiil na nafasi yake kwa Imamu Hussein (a.s), jinsi alivyokua anaaminika kwa Imamu Hussein tofauti na watu wengine, na akamfanya kua balozi wake (a.s) pia shekh akaelezea tukio la kifo chake.
Majlis ikafungwa kwa kusoma kaswida na tenzi za huzuni kuhusu msiba huu ulio umiza roho ya Imamu Hussein (a.s) na za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).