Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad yahitimisha mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu –tawi la Bagdad- chini ya Atabatu Abbasiyya imehitimisha mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi, imefanya hafla katika maeneo tofauti ya Bagdad kwa ajili ya kuwapongeza wahitimu wa semina hizo wapatao (4500).

Mahafali hizo zimepata mahudhurio makubwa ya viongozi wa Dini, wasomi wa Qur’ani pamoja na viongozi wa kijamii, bila kuzisahau familia za wanafunzi ambao wametoa pongezi nyingi kwa Ataba tukufu kutokana na mambo mbalimbali inayo fanya, likiwemo hili la semina za Qur’ani ambazo zimetoa mchango mkubwa sana katika sekta ya Qur’ani ndani na nje ya Iraq, wakasema: Leo tunaona matunda ya Ataba kwa kusherehekea kuhitimu kwa vijana wetu, ambapo wamesomeshwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na Qur’ani, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu pamoja na kuendesha semina hizi pia husimamia vikao vya usomaji wa Qur’ani sehemu mbalimbali, na huwapa kipaombele zaidi watoto na vijana wenye vipaji vya usomaji wa Qur’ani, huwawekea ratiba ya kukuza vipaji vyao na huwapa kila kinacho hitajika, pia hushirikiana na taasisi zingine za Qur’ani kwa ajili ya kubadilishana uzowefu, na hushiriki katika mashindano na makongamano ya kitaifa na kimataifa, hali kadhalika huandaa mubalighina (walimu) katika somo ya Qur’ani kwa kutoa semina za kujenga uwezo kwa wakufunzi wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: