Mahudhurio makubwa yanayo kadiriwa zaidi ya laki ya mazuwari yameshuhudiwa katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kwenye eneo la katikati yake siku ya Jumapili (9 Dhulhijja 1440h) sawa na (11 Agost 2019m), watu walianza kuwasili katika maeneo haya matakatifu tangu mapema leo asubuhi hadi wakati wa kuandikwa habari hii bado wanaendelea kuwasili, kwa ajili ya kuhuisha na kufanya ibada za siku ya Arafa.
Wamefanya ibada za siku ya Arafa ndani ya Ataba mbili tukufu na katika eneo la katikati ya haram mbili, miongoni mwa ibada hizo ni kufanya ziara katika malalo mawili matukufu, ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wameendelea kufanya ibada kuanzia asubuhi hadi jioni kisha watafanya ibada maalum za usiku wa Iddi na hapo kesho watafanya ibada za mchana wa Iddi, hii ni moja ya ziara ambazo huhudhuriwa na watu wengi.
Nazo Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetumia uwezo wake wote katika kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuwapa huduma bora kabisa mazuwaru hao waliokuja kutoka ndani na nje ya taifa, ulinzi umeimarishwa na vituo vya afya vimejipanga vizuri.
Fahamu kua miongoni mwa ibada za leo ni kusoma Qur’ani tukufu na dua ya siku ya Arafa iliyo pokewa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) pamoja na dua zingine zilizo pokewa kutoka kwa Ahlulbait (a.s) sambamba na ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).