Kitengo cha kulinda nidhamu kimeweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha usalama katika siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha tukufu.

Maoni katika picha
Kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeweka mkakati maalum wa kuimarisha usalama katika siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha na kuhakikisha mazuwaru wanatembea kwa amani na utulivu.

Watumishi wa kitengo hicho wamesambazwa vituoni kutekeleza mradi huo, pamoja na kusaidiwa na wahudumu wa kujitolea, ambao wamepangwa kusaidia kuratibu uingiaji na utokaji katika milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya ulinzi mkali, sambamba na kuandaa mazingira bora ya kufanya ziara na ibada zingine kwa amani na utulivu, hii ndio desturi ya watumishi wa Ataba tukufu katika kila ziara inayo hudhuriwa na watu wengi, mazuwaru walianza kuwasili kwa wingi tangu asubuhi ya siku ya Jumapili.

Kumbuka kua miongoni mwa ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi katika mji wa Karbala ni ziara ya siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha, waumini huja kwa wingi kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara maalum ya siku ya Arafa, usiku wa Iddi na mchana wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: