Katika mazingira yaliyo jaa utulivu: Waumini wanaswali Iddi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Katika mazingira tulivu na roho zilizo jaa mapenzi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na baada ya watu kumiminika katika mji wa Karbala wakitoka ndani na nje ya Iraq, kuja katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kufanya idaba za usiku na mchana wa Arafa wanahitimisha kwa swala ya Iddi tukufu, imehudhuriwa na watu wengi sana, haram imejaa watu wanaoswali ndani na nnje.

Swala ya Iddi imeswaliwa katika haram zote mbili, ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi imeswaliwa zaidi ya mara moja, kutokana na wingi wa watu waliokuja kuswali na udogo wa eneo, na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu pia ulifurika watu walio swali chini ya uimamu wa Shekh Habibu Alkadhimiy.

Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo katika kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhakikisha inatoa huduma bora kwao, vyombo vya ulinzi na usalama viliimarisha ulinzi na kuhakikisha mazuwaru wanatekeleza ibada kwa utulivu na amani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: