Idara ya mahusiano na vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu yasaidia katika ratiba maalum ya matibabu siku ya Arafa na siku ya Idul-Adh-ha

Maoni katika picha
Idara ya mahusiana na vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha mahusiano, kwa kushirikiana na idara ya madaktari na waokozi wa kivita, wameshiriki katika ratiba maalum ya Idul-Adh-ha iliyo pangwa na uongozi mkuu wa Ataba tukufu.

Idara imetumia wanafunzi kutoka vyuoni na kwenye Maahadi za hapa Iraq, wenye mafunzo ya utowaji wa huduma za uokozi, wamekuja kutoa huduma za kitabibu katika siku ya Arafa na Idul-Adh-ha, watu wanaotoa huduma za kitabibu hufanya kazi saa (24), wameweka kambi katika barabara kuu zinazo elekea haram na karibu ya malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiwa na gari za wagonjwa za Atabatu Abbasiyya, wako tayali kutoa huduma za haraka kwa mtu yeyote atakaye patwa na tatizo la kiafya, kutokana na msongamano wa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua kikosi cha watu wanao toa huduma za matimabu ni madaktari, wanafunzi wa udaktari na wauguzi wote wanajitolea, baadhi yao walipewa mafunzo ya uokozi na wengine ni wakongwe katika kazi hiyo, wana vifaa tiba vyote vinavyo hitajika, jukumu lao ni kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru na uokozi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: