Kwa kushirikiana na viundi vya wakina mama: Idara ya Zainabiyyaat katika Atabatu Abbasiyya yafanya kazi kubwa katika usiku wa Arafa na Iddi pamoja na michana yake

Maoni katika picha
Idara ya Zainabiyyaat katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na vikundi vingine vya wakina mama kutoka Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya na maelekezo ya kidini tawi la wanawake, wamefanya kazi kubwa katika usiku wa Arafa na Iddi pamoja na michana yake, kwa kiasi ambacho mazuwaru wa kike wamefanya ibada zao kwa amani na utulivu bila usumbufu wowote, katika sehemu walizo pangiwa ndani ya haram na katika sardabu (sardabu ya Imamu Hussein na Imamu Jawaad –a.s-, pamoja na kwenye sardabu ya Alqamiy na ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Hakika ziara ya usiku wa Arafa na Iddi pamoja na michana yake ni kielelezo halisi cha kazi nzuri waliyo fanya, na huo ni muendelezo wa utendaji mzuri walio nao katika ziara ya Ashura, Arubaini, Shaábaniyya pamoja na siku za Ijumaa katika kila wiki.

Idara ya Zainabiyyaat pamoja na idara zingine ilizo shirikiana nazo zimeratibu vizuri matembezi ya mazuwaru, zimetoa mawaidha na maelekezo ya kidini kwao, na zimesimamia swala za jamaa ndani ya haram, pia zimeendesha swala ya jamaa nyingine ndani ya Sardabu, wamefanya mambo mengi mazuri nafasi haitoshi kuandika yote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: