Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wapeleka dirisha la Qassim (a.s) kwenye malalo yake

Maoni katika picha
Baada ya mafundi wa kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi na mazaru tukufu kukamilisha utengenezaji wa dirisha la kaburi la Qassim bun Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s), msafara umeondoka Karbala ukielekea katika mji wa Qassim (a.s), ambako dirisha jipya limepokelewa kwa shangwe na vifijo na wakazi wa mji huo na wamechinja (mbuzi na kondoo kuonesha furaha yao) mbele ya dirisha hilo, linalo ashiria utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tumeongea na kiongozi aliye simamia utengenezaji wa dirisha hilo Mhandisi Ali Salum amesema kua: “Baada ya kukamilisha uundwaji wa dirisha la Qassim bun Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s) katika kiwanda maalum cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kinacho husika na kutengeneza madirisha na milango ya kwenye malalo na mazaru tukufu, hii ni kazi nzuri inayo fanywa na Ataba tukufu baada ya kufanikiwa kutengeneza dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasema: “Wakati wa kuleta dirisha hili tumepata mapokezi makubwa kutoka kwa wakazi wa mji huu, watu wa mji huu wana moyo wa kujitolea kwa ajili ya taifa lao na maeneo matakatifu, pia mji huu unamashahidi wengi walio uwawa katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh, leo wanaonyesha mapenzi yao katika kupokea dirisha la malalo ya Qassim (a.s)”.

Akabainisha kua: “Dirisha hili limesanifiwa na kutengenezwa na watalam wa kiiraq, hali kadhalika aya za Quráni zilizopo kwenye dirisha hili zimetengenezwa na watalam wa hati wa kiiraq, limetumia karibu kilo (522) za fedha, na karibu kilo (13) za dhahabu, pamoja na kilo (2000) za kopa na kilo (2500) za chuma kigumu, aidha zimetumika aina bora kabisa za mbao, kazi imekamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa, kazi hii inaingia katika orodha ya mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Fahamu kua kazi ya kutengeneza madirisha na kuyaweka sehemu zake sambamba na kuondoa madirisha ya zamani inafanywa na Atabatu Abbasiyya kupitia kiwanda cha Saqaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: