Mafundi wa kiwanda cha Saqaa kinacho husika na kutengeneza madirisha na milango ya kwenye malalo na mazaru tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya siku ya Jumanne (12 Dhulhijja 1440h) sawa na (13 Agost 2019m), wamemaliza kutoa dirisha la zamani katika mazaru wa Qassim bun Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s), ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mkataba uliowekwa kati ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya na uongozi mkuu wa mazaru hii tukufu, sasa kazi ya kuweka dirisha jipya lililo zinduliwa hivi karibuni itaanza.
Yanajiri haya baada ya mapokezi makubwa yaliyo fanywa na watu wa mji huu, katika kupokea dirisha jipya lililoletwa kutoka Karbala, wakazi wa mji wa Qassim wamepokea dirisha hilo kwa shangwe na vifijo pamoja na kuchinja kama ishara ya kilele cha furaha yao kwa jambo hilo.
Mkuu wa kiwanda cha Saqaa amesema kua: “Tumemaliza kazi tuliyo pewa ya kutengeneza dirisha jipya la mazaru ya Qassim (a.s), tumemaliza kufungua dirisha la zamani na kulisafisha kisha tumelikabidhi kwa uongozi mkuu wa mazaru ya Qassim (a.s)”.
Kumbuka kua dirisha jipya la mazaru hii limeingizwa katika orodha ya mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayo pata kupitia mafundi na watalamu halisi wa kiiraq.