Kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetumia gari zake zote katika kipindi cha Iddul-Adh-ha na kwenye siku ya Arafa

Maoni katika picha
Kitengo cha usafiri chini ya Atabatu Abbasiyya kinaendelea na kazi zake za kubeba mazuwaru wa bwana wa mashahidi na Abulfadhil Abbasi (a.s) bure, kutoka haram hadi barabara ya Imamu Hussein (a.s), kazi za kitengo hiki huongezeka katika siku za ziara kubwa na siku za Iddi pamoja na siku zenye matukio muhimu kidini, kitengo kimetumia gari zake zote kubeba mazuwaru katika siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha.

Makamo rais wa kitengo cha usafiri Ustadh Maitham Adbul-Amiir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kitengo cha usafiri kinafanya kazi saa (24), tunabeba mazuwaru kutoka haram hadi kwenye barabara ya Kiblq ya Imamu Hussein (a.s) kwa kupitia barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika siku hizi tumekua tukiangalia mazingira ya barabara zinazo elekea kwenye haram mbili tukufu, tukiona msongamano wa mazuwaru sehemu yeyote tulikua tunaagiza gari na kuja kuwabeba, wala hakuna tatizo lililo tokea katika barabara zote zinazo elekea kwenye haram takatifu”.

Akaongeza kua: “Tuna gari nne za wagonywa ambazo zilikua tayali kutoa huduma muda wote katika ziara ya Arafa, na bado zinaendelea kutoa huduma hadi mwisho wa siku ya Iddi, zimesaidia kubeba wagonjwa wengi na kuwapeleka hospitali za jirani na baadhi yao wamepelekwa kwenye hospitali ya Husseiniy”.

Akasema: “Gari za kusambaza maji zimefanya kazi kubwa siku ya Arafa na Iddi, tumegawa maji safi ya kunywa katika mawakibu zilizopo ndani na nje ya mji wa Karbala, sambamba na vituo vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: