Kituo cha afya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu: kimetoa huduma za matibabu saa (24) katika ziara ya Arafa na siku ya Iddul-Adh-ha

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu hujitahidi kufanya kila kitu kinacho hitajiwa na zaairu katika kipindi cha ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi, ikiwa ni pamoja na huduma zi kiafya.

Katika siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha kituo chake cha afya kimefanya kazi saa (24).

Kituo hicho kinatoa huduma za dharura kwa mazuwaru wanaopatwa na maradhi wakati wa kufanya ziara kutokana na msongamano au matatizo mengine, hupewa matibabu yanayo endana na maradhi yao.

Kama tatizo likiwa kubwa hupelekwa katika hospitali za karibu kwa matibabu zaidi, kazi hiyo hufanywa kwa kushirikiana na uongozi wa afya wa mkoa wa Karbala.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalum kwa ajili ya ziara ya siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: