Mafundi wa kiwanda cha Saqaa wanaendelea na kazi ya kufunga dirisha jipya katika mazaru ya Qassim bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kwa siku ya pili mfululizo, wameanza kufunga majengo ya mbao kisha wataweka vipande vilivyo tengenezwa kwa dhahabu na kutiwa mina.
Kiongozi wa kiwanda cha Saqaa Sayyid Nadhim Algharabi ameeleza utenda wao kua: “Kazi ya kufunga dirisha katika mazaru ya Qassim (a.s) inaendelea vizuri, tunatarajia kumaliza kazi hii kabla ya kuingia mwezi mtukufu wa Muharam”.
Akaongeza kua: “Kazi hii inahusisha uwekaji wa maandishi ya Quráni na mashairi yaliyo andikwa kwa dhahabu pamoja na nakshi zilizo tiwa dhahabu”.
Kumbuka kua dirisha tukufu la mazaru ya Qassim (a.s) limetengenezwa katika kiwanda cha Saqaa, kinacho husika na utengenezaji wa madirisha na milango ya kwenye malalo na mazaru takatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.