Kila kitu kitaondoka

Maoni katika picha
Kila kitu kitaondoka, ispokua vitendo vyema vitahifadhiwa katika daftari la vitendo, kwa hiyo vitende vyema ni hazima ya uhakika, jitahidi kufanya mema hakika hakuna anayejua ukubwa wake ispokua Mwenyezi Mungu, kama ukiangalia kwa undani utakuta kua kimbunga cha mahabba ni mlango mkubwa wa rehema za Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu mtukufu huwapenda sana watu wanao onyesha upendo kwa viumbe wake, mapenzi hayo huwa mara dufu kwa kuwapenda watu walio chini ya Imamu Hussein na ndugu yake mwezi wa bani Hashim (a.s).

Katika siku ya mwisho ya sikukuu ya Iddul-Adh-ha, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimekutana na kundi la waumini katika kusherehekea sikukuu hii mbele ya malalo takatifu, na wamenyanyua mikono na kuomba dua ya kukidhiwa haja zao na kumuomba Mwenyezi Mungu awakutanishe na siku kama ya leo mwakani.

Bado vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinaendelea na kazi ya kuwahudumia mazuwaru watukufu, na kuhakikisha wanafanya ziara kwa amani na utulivu, siku mbili baada ya Iddi hutarajiwa kuwa na ongezoko kubwa la watu wanaokuja kufanya ziara katika mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: