Kwa picha: Kazi ya kufunga dirisha jipya katika mazaru ya Qassim (a.s) inaendelea

Maoni katika picha
Kazi ya kufunga dirisha katika mazaru ya Qassim bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s) inaendelea kwa siku ya tatu mfululizo, kazi hiyo inafanywa na mafundi wa kiwanda cha Saqaa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa kiwanda cha Saqaa amesema kua: “Kazi ya kufunga dirisha jipya katika mazaru ya Qassim (a.s) inaendelea kwa siku ya tatu mfululizo, tayali herufi za Quráni kutoka surat Nuur na herufi za mashairi zimewekwa”.

Akaongeza kua: “Tumemaliza kuweka kibalaza cha msingi wa dirisha pamoja na vipande vilivyo nakshiwa kwa dhahabu, sambamba na kuweka herufi za mashairi”.

Fahamu kua dirisha la mazaru ya Qassim bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s), ni miongoni mwa mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kiwanda cha Saqaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: