Uongozi wa hospitali ya rufaa Alkafeel: Hospitali imesaidia maelfu ya wanamchi, kiwango cha misaada kinakaribia trilioni (4) dinari za Iraq

Maoni katika picha
Miongoni mwa vipengele vya kongamano la kwanza la kuwazawadia madaktari wa Iraq, linalo simamiwa na hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kulikua na ujumbe maalum wa hospitali ulio wasilishwa na mkuu wa hospitali hiyo Dokta Jaasim Ibrahimi alasiri ya Ijumaa (14 Dhulhijja 1440h) sawa na (16 Agost 2019m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Katika ujumbe huo Dokta Ibrahimi amesema: “Uongozi wa hospitali ya rufaa Alkafeel katika mji wa Karbala, unashukuru viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutusaidia kufanya kongamano hili, msaada huu ni sehemu ndogo sana ya msaada endelevu tunao pewa kila siku, unao tuwezesha kutekeleza majukumu yetu ipasavyo na miongoni mwa mambo tuliyo fanikiwa kuyafanya ni:

Kwanza: Hospitali ya rufaa Alkafeel imekua moja ya nguzo muhimu katika kusaidia raia, hasa wasio kua na uwezo wa kutibiwa katika hospitali binafsi, hospitali ya Alkafeel ilisimama imara kuwasaidia watu walio jeruhiwa katika vita dhidi ya Daesh pamoja na kusaidia maelfu ya wananchi kwa kiasi kinacho karibia trilioni (4) dinari za Iraq.

Pili: Hospitali ya rufaa Alkafeel imefanikiwa kuwa mshirika mkubwa wa wizara ra afya na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, hospitali inatoa huduma nzuri kwa kiwango cha juu, na inapigiwa mfano katika ubora.

Tatu: Utowaji wa mafunzo, imekua kituo maalum cha mafunzo kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed cha Karbala.

Nne: Kuanzisha na kutoa huduma mpya kama kupandikaza figo na zinginezo.

Tano: Kujenga uhusiano mzuri na wafanya kazi na kuwashajihisha katika utendaji wao kwa kuwawekea mfumo mzuri wa kiidara unaofuata kanuni za utawala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: