Jopo la madaktari wa kiiraq katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefaulu kumtibu mtoto mwenye umri wa miezi mitatu aliyekua na tatizo la moyo

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa Iraq katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefanikiwa kutibu mtoto mwenye umri wa miezi (3) aliye kua anasumbuliwa na maradhi ya moyo.

Kiongozi wa jopo la madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo katika hospitali ya Alkafeel Dokta Ahmadi Abudi amesema kua: “Jopo la madaktari limefanikiwa kimtibu mtoto aliye kua na kilo nne huku akiwa na umri wa miezi mitatu tatizo alilokua nalo katika moyo wake, naye ni mkazi wa Bagdad”.

Akaongeza kua: “Kazi ya upasuaji imechukua saa nne, ilikua kazi hatari kwa sababu mtoto alikua dhaifu na mwenye uzito mdogo, lakini hali yake kiafya ililazimika afanyiye upasuaji huo”.

Fahamu kua upasuaji huu ni miongoni mwa kazi zenye mafanikio katika upasuaji wa moyo kwenye hospitali ya Alkafeel, umesha fanyika upasuaji wa moyo mara nyingi kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja na wenye uzito tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: