Ustawi wa jamii katika Masjid Aali Yaasin: Sikukuu yetu kuwa pamoja na wapiganaji katika uwanja wa ushindi na utukufu

Maoni katika picha
Pamoja na kuwepo kwa joto na umbali lakini kikosi cha watumishi wa ustawi wa jamii katika msikiti wa Aali Yassin katika mkoa wa Bagdad chini ya ofisi ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya iliamua kuwa pamoja na wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika maeneo yaliyo chini ya Liwaau/44 Hashdi Shaábi kwenye mji wa Hadhar mkoa wa Mosul, wakiwa na zawadi mbalimbali, na kuthibitisha kua sikukuu ina chakula maalum na furaha yao ni kula pamoja na ndugu zao wapiganaji.

Msafara huu unatokana na maelekezo ya wakili wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya, umebeba aina tofauti za vyakula ambavyo wamegawa kwa wapiganaji hao.

Wapiganaji wameshukuru sana kutembelewa na kupewa msaada huo na wametuma shukrani rasmi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa namna inavyo wajali na kuwasaidia wakati wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: