Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unaangalia hatua iliyo fikiwa katika kufunga dirisha jipya la mazaru ya Qassim (a.s)

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umetembelea mazaru ya Qassim bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s), kuangalia hatua iliyo fikiwa katika kufunga dirisha jipya la mazaru hiyo.

Kiongozi wa kiwanda na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Kadhim Abbada ameuambia mtandao wa Alkafeel sababu ya ziara hiyo: “Leo tumetembelea malalo ya Qassim bun Imamu Mussa bun Jafari (a.s), kuangalia maendeleo ya kazi ya kufunga dirisha tukufu, lililo undwa katika kiwanda cha Saqaa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasema: “Tumekuta kazi inaendelea vizuri, mafundi wamefanya kazi kubwa kwa muda mfupi, inaonyesha kua kazi itakamilika ndani ya muda uliopangwa”.

Akaongeza kua: “Kazi ya kufunga dirisha itakamilika ndani ya siku chache zijazo Insha Allah, na dirisha litafunguliwa mbele ya mazuwaru”.

Kumbuka kua katibu maalum wa mazaru hiyo bwana Karim Hussein aliongozana na ugeni wa Ataba tukufu wakati wa matembezi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: