Jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea zaidi ya wanachama (60) wa Skaut kutoka mji wa Diwaniyya, na imewaweka katika hema la Skaut lililo pewa jina la (Hema la Muslim bun Aqiil –a.s-) sambamba na ratiba ya mafunzo ya kujenga uwezo yanayo endelea hivi sasa, kiongozi wa ratiba za hema katika idara ya watoto Ustadh Ali Hussein Abdu Zaid amesema kua: “Hema hili ni sehemu ya harakati za idara kwa kukaribisha wanachama wa Skaut kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, watakaa siku tatu mfululizo na watafundishwa mambo tofauti ikiwa ni pamoja na ratiba za nichezo”.
Akaongeza kua: “Ratiba imeanza kwa kufanya hafla kubwa ndani ya ukumbi uliopo katika jengo la Shekh Kuleini, kwa kuwakaribisha wageni watukufu na halafu ikafunguliwa kwa Quráni takatifu, kisha likafanyika onyesho la igizo, na kuhitimisha kwa maswali mbalimbali ya Aqida na Quráni pamoja na mashindano ya kielimu na hapo ukawa mwisho wa ratiba ya siku ya kwanza”.
Akafafanua kua: “Wanafunzi walikua na hamasa kubwa katika utekelezaji wa ratiba ya masomo, ni muhimu sana mtu kua na shauku ya kuongeza uwezo wake kielimu na kiakili sambamba na kushikamana na mafundisho ya Ahlulbait (a.s)”.