Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo mazuri kwa ajili ya kusherehekea Idul-Gadiir

Maoni katika picha
Mazingira ya shangwe na furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia kumbukumbu ya Idul-Ghadiir, kuta zimewekwa mabango yaliyo andikwa maneno yanayo onyesha upendo na utiifu kwa kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kama kielelezo cha furaha kubwa iliyojaa ndani ya nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kumbukumbu ya kutangazwa kwake kama kiongozi wa waumini na khalifa wa Mtume (s.a.w.w).

Kama kawaida, Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum kwa ajili ya tukio hilo tukufu, kutakua na vikao pamoja na mawaidha ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na mahafali zitakazo fanywa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Kumbuka kua siku ya mwezi kumi na nane Dhulhijja mwaka wa kumi hijiriyya, Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) alitangazwa kua kiongozi wa waumini na khalifa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: