Katika awamu ya kumi na mbili… kongamano la mwezi laandaa ratiba ya kitamaduni kwa wanafunzi (43) kutoka Baabil

Maoni katika picha
Katika awamu ya kumi na mbili ya kongamano la mwezi linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imeandaliwa ratiba kwa wanafunzi (43) kutoka katika mkoa wa Baabil kwenye shule za sekondari na vyuo.

Wameandaliwa ratiba kamili inayo husisha masomo ya Aqida na kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ustadh Farasi Shimri mmoja wa wakufunzi katika ratiba hiyo ameuambia mtandao wa Alkafuul kua: “Ratiba hii itachukua siku nne (4), kutakua na mihadhara ya mambo mbalimbali kama vile: (kujitegemea, changamoto za vifaa vya elektronik upande wa sharia na adhabu zake pamoja na mihadhara ya Aqida, na mambo mengingine yenye utata), pia kunaratiba ya kutembelea hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kua kongamano la mwezi ni kongamano la kielimu na kitamaduni linalenga tabaka tofauti za watu katika jamii, kwa ajili ya kupambana na changamoto za kidini na kitamaduni, na kujibu changamoto hizo kwa kutumia elimu kwa kutumia hoja bila chuki na ugonvi, mambo ambayo huleta madhara makubwa katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: