Miongoni mwa harakati zake katika maswala ya Quráni, Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha semina chini ya anuani isemayo (Uandishi wa tafiti za kielimu kisasa katika masomo ya Quráni na Aqida), semina hiyo inamasomo mengi na mihadhara tofauti inayo eleza namna ya kuendeleza masomo ya Quráni, yote hayo yapo ndani ya mkakati wa Maahadi ya Quráni tawi la Najafu.
Muhadhara wa kwanza ulio tolewa na Dokta Ammaar Abdurazaaq Swaghiir ulikua unahusu utambuzi wa mitazamo ya kitafiti, kaeleza utafiti na malengo yake, pamoja na namna ya kusoma na hatua muhimu za kubaini tatizo na misingi yake, akataja vitu muhimu kinadhariyya vinavyo husiana na mtafitu pamoja na utafiti, sambamba na kufafanua baadhi ya mahitaji, aidha ametoa ushahidi wa vitu anavyo weza kukutana navyo mtafiti katika uandishi wa tafiti za kielimu.
Muhadhara ulipata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi na washiriki wote kwa ujumla kutokana na umuhimu wa mada hiyo katika kupambana dhidi ya fikra potofu zinazo chafua Imani ya kiislamu.
Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya haijawahi kuacha kufanya harakati zinazo husiana na Quráni tukufu kuanzia usomaji, kuhifadhi na kuifanyia utafiti.