Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yawa mwenyeji wa kikao cha usomaji wa mashairi katika kumbukumbu ya Idul-Ghadiir

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya jioni ya siku ya Jumanne (18 Dhulhijja 1440h) sawa na (20 Agost 2019m) kimefanya kikao cha usomaji wa mashairi kwa wanawake katika kusherehekea kumbukumbu ya Idul-Gadiir na kushiriki jopo la washairi na waimbaji wa Husseiniyya.

Kongamano hilo limefanyika ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru waliokuwepo ndani ya haram tukufu na ikawa ni fursa ya kushiriki kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika furaha hizo kutoka kila sehemu ya dunia.

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha zikafuara tenzi na mashairi mbalimbali, halafu akapanda kwenye jukwaa Hussein Abu Iraq, kisha Muhammad Fatwimiy na Muhammad Aájami, wakasoma mashairi yanayo onyesha mapenzi na utiifu kwa mbora wa mawasii Imamu Ali bun Abu twalib (a.s), aidha naye muimbaji mahiri Thaamir Aaridhi alikua na nafasi maalum ya kuimba katika hafla hiyo.

Kumbuka kua siku ya mwezi 18 Dhulhijja ni kumbukumbu ya Idullahi Akbaru, Idul-Ghadiir nayo ni siku aliyo tangazwa Ali bun Abu Twalib (a.s) kua kiongozi wa waumini na mbora wa mawasii na khalifa wa Mtume (s.a.w.w), wafuasi wa Ahlulbait (a.s) koto duniani huadhimisha siku hiyo tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: