Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na vikao vya kongamano la tatu kwa siku ya nne mfululizo, ratiba ya jana Jumatano (19 Dhulhijja 1440h) sawa na (21 Agost 2019m) ilikua na muhadhara usemao: (Kujenga kujiamini katika kushinda changamoto), ambapo zilizungumziwa mbinu za kupambana na changamoto mbalimbali katika maisha ya kila siku.
Likafuatiwa shindano la mambo ya kitamaduni kati ya kikundi cha Ameed na Saaqi, kipengele cha tatu kilikua kinahusu kazi zinazo mfaa mwanadamu katika maisha yake, na mwisho wakapewa mafunzo ya namna ya kutoa huduma ya kwanza katika uokozi.
Fahamu kua kongamano hili litafanyika kwa siku tano mfululizo, linalenga kuongeza uwelewa katika masomo ya Fiqhi, Aqida na mambo mengine.
Kumbuka kua kituo kipo Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Hussein (a.s) ndani ya jengo la Swidiqah Twahirah (a.s), kinatoa huduma kwa wanchi wote wa Iraq, hasa wakazi wa mkoa wa Karbala, kwa maelezo zaidi piga simu namba (07828884555), namba hiyo pia inapatikana kwenye (Viber, Whatsapp na Telegram) au unawaweza kujiunga katika kituo cha utamaduni wa familia kwa kupitia link ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1.