Siku ya Alkhamisi (20 Dhulhija 1440h) sawa na (20 Agost 2019m), Ugeni kutoka ubalozi wa Iraq nchini Holandi ukiongozwa na Mheshimiwa balozi Dokta Hisham Alawiy umetembelea shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Aljuud ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia miradi ya Ataba na maendeleo yaliyo patikana katika sekta tofauti.
Ugeni huo umetembelea sehemu mbalimbali za kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na sehemu ya uzalishaji wa bidhaa za kilimo na viwandani.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Ustadh Maitham Bahadeli ametoa maelezo kuhusu vitengo vya uzalishaji na bidhaa wanazo tengeneza, ugeni umepongeza kazi nzuri zinazo fanywa na shirika la Aljuud, kwani limekua shirika linalo tegemewa katika sekta ya vifaa vya kilimo na viwanda, kutokana na ubora mkubwa wa bidhaa zake.
Mwishoni mwa matembezi yao wakaomba kuwe na ushirikiano baina ya shirika la Aljuud na vituo vya utafiti vya Holandi, balozi akaahidi kua atachukua jukumu la kueleza maendeleo aliyo yaona katika shirika la Ajuud katika sekta ya viwanda na kilimo.