Kituo cha utamaduni wa familia chahitimisha kongamano lake la tatu la wanafunzi wa sekondari

Maoni katika picha
Alkhamisi ya jana (21 Dhulhijja 1440h) sawa na (22 Agost 2019m) kongamano la latu la wanafunzi wa sekondari limefika tamati, chini ya kituo cha utamaduni wa familia cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala.

Kongamano hilo limefanyika kwa muda wa siku tano mfululizo lilikua na vipengele vingi vinavyo lenga kufundisha elimu na utamaduni, na limehitimishwa kwa mada ya Aqida kuhusu utukufu wa Mwenyezi Mungu na uadilifu wake, na mada nyingine ilikua inahusu historia ya Mtume (s.a.w.w).

Kisha yakafuata maswali na majibu kuhusu Imamu Mahadi ambayo ilikua mada ya siku ya pili ya kongamano.

Kikosi cha uimbaji cha madrasat Fadak Zaharaa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kilikua na ushiriki maalum katika hafla hiyo, wameimba kaswida kuhusu bibi Fatuma Zaharaa (a.s) pamoja na kugawa zawadi kwa wageni waalikwa.

Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim amesema kua: “Mwaka kesho tutakua na mpango mpya unao endana na mahitaji ya tabaka la vijana kitamaduni, kijamii na kimaadili sambamba na kuchunga mipaka ya sheria zetu tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: