Ugeni kutoka Maahadi ya Quráni tukufu unakutana na rais wa chuo kikuu cha Dhiqaar, na chuo hicho kimeonyesha utayali wa kushirikiana na Maahadi

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya ziara maalumu katika mradi wa kufundisha Quráni kwenye nyuo na Maahadi za Iraq, ugeni kutoka Maahadi ya Quráni tukufu umekutana na rais wa chuo cha Dhiqaar Dokta Yahaya Abduridhwa Abbasi, ambaye amesema kua mradi huo ni hatua kubwa na unamalengo mazuri.

Rais wa chuo hicho ameonyesha utayali wa kushirikiana na Maahadi, amesema kua: “Chuo cha Dhiqaar pamoja na kila ilicho nacho, kipo tayali kutoa msaada wowote utakao hitajika katika mradi huu”.

Nao wageni kutoka Maahadi ya Quráni tukufu wakaeleza malengo ya mradi na nyanja za kushirikiana kielimu na kitamaduni, na mambo yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika vyuo na Maahadi za Iraq kwa ajili ya kuweka mazingira ya Quráni, elimu na Aqida iliyojengwa katika msingi sahihi ya kiislamu, inayo tokana na uwelewa wa kina wa Quráni tukufu sambamba na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia utowaji wa mafunzo na mashindano.

Fahamu kua kituo cha miradi ya Quráni tukufu katika Maahadi ya Quráni chini ya Atabatu Abbasiyya huendesha miradi mbalimbali ndani ya mwaka mzima, na hulenga watu wa umri na elimu tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: