Mradi wa kijana wa Alkafeel kitaifa waweka wanafunzi katika hema la Skaut

Maoni katika picha
Mradi wa kijana wa Alkafeel kitaifa katika idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na Atabatu Abbasiyya tukufu, umeingiza wanachama wake miongoni mwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi za Iraq katika hema la Skaut liitwalo (Hema la kijana wa Skaut), kwa mwaka wa saba mfululizo, wameshiriki wanafunzi wa mikoa na Maahadi tofauti, ukizingatia wao ndio mabalozi wa mradi katika taasisi hii.

Hema hilo limewekwa katika ukumbi wa chuo kikuu cha Al-Ameed kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya uhusiano Ustadh Maahir Khalidi: “Ni sehemu ya kukamilisha ratiba ya hema na kuendeleza mafanikio mazuri yanayo patikana kwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi hapa Iraq, na kudumisha mawasiliano baina ya Atabatu Abbasiyya na taasisi zingine pamoja na kuendeleza harakati za Dini na utamaduni, ratiba ina vitu vingi, yakiwemo mafundisho ya Dini, utamaduni na michezo”.

Akaongeza kua: “Katika hema hilo wameshishiki zaidi ya wanafunzi (70) kutoka mikoa ya kati na kusini pamoja na mji mkuu wa Bagdad, wote wakiwa ni wanachama wa mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel katika vyuo vikuu vya Iraq, ratiba imeandaliwa na kamati ya watalamu na inatekelezwa na watu walio bobea katika kuamiliana na watu wa aina hiyo, kulikua na mihadhara ya Fiqhi, Aqida pamoja na michezo, bila kusahau mashindano ya kidini na kitamaduni, kulikua na maswali ya Fiqhi, Aqida, Sayansi, Historia, Jografia na Lugha, na mihadhara ya maendeleo ya kibinadamu, sambamba na mijadala huru kuhusu hali ya taifa, pamoja na kutembelea baadhi ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake, na kutembelea Maraajii watukufu katika mji wa Najafu na Ataba takatifu zilizopo katika mji huo”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inasimamia program nyingi za kielimu na kitamaduni ndani na nje ya Ataba tukufu zinazo lenga wanafunzi, kwa ajili ya kufundisha misingi ya Dini ya kiislamu, kwa kufuata mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), na kujenga uzalendo wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: