Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya hafla ya mwisho wa mwaka ya kwanza katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zake za kuitumikia Quráni tukufu, Maahadi ya Quráni tawi la mkoa wa Najafu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya, kwa kushirikiana na kituo cha miradi ya Quráni wamefanya hafla ya kwanza ya mwisho wa mwaka wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa ndani ya ukumbi mkuu wa Alawiyya na kuhudhuriwa na taasisi za Quráni katika mkoa huo pamoja na ugeni kutoka Atabatu Alawiyya.

Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na mwanafunzi wa mradi wa kitaifa Hafidhi Khaliil Ismaili, likafuata neno la ukaribisho kutoka kwa kiongozi wa tawi hilo katika mkoa wa Najafu Sayyid Muhandi Almiyahi, amekaribisha wageni wote walio hudhuria na kumshukuru kila aliye changia kufanikisha hafla hiyo.

Akaendelea kusema: “Hakika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa ni moja ya miradi muhimu inayo fanywa na kituo cha miradi, na sisi hapa Najafu tumefanya sehemu ya mradi huo na kuhusisha idadi kadhaa ya madrasa za usomaji wa Quráni, na tukaandaa ratiba mahsusi ya watoto wenye vipaji vya usomaji hapa Najafu”.

Baada yake ukafuata usomaji wa kikundi cha madrasa ya Shekh Shahata Muhammad Nuur cha kiwango cha tamhidi (awali) katika tawi na Najafu, kisha akasoma Abbasi Haadi mmoja wa wanafunzi wa madrasa ya Shekh Muhammad Swidiiq Minshawi, halafu mwana kikundi Hussein Abdulkarim mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji katika mji wa Najafu akasoma kwa mahadhi ya Kiiraq, hafla ikahitimishwa kwa kisomo cha pamoja cha wanafunzi wa madrasa ya Shekh Abdulfataah Shaáshaí, kisha wale wote walio soma wakapewa vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: