Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika kongamano la Idul Ghadiir kwenye uwanja wa haram tukufu ya Alawiyya

Maoni katika picha
Jioni ya siku ya Jumapili (23 Dhulhijja 1440h) sawa na (25 Agost 2019m) lilifunguliwa kongamano la Idul Ghadiir linalo simamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Alawiyya, na kuhudhuriwa na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliokua na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na wakuu wa baadhi ya vitengo.

Hafla imehudhuriwa na viongozi wengi wa Dini, sekula na wanahabari kutoka ndani na nje ya Iraq, pamoja na mazuwaru, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya ulio tolewa na katibu mkuu Mhandisi Yusufu Shekh Radhi, ambaye alielezea utukufu wa siku ya Ghadiir na athari yake kihistoria, na vipi tukio hilo muhimu limepambanua watu na kubainisha njia ya haki, akaeleza pia kuhusu mradi wa kuweka dhahabu katika mnara wa kusini mwa uwanja wa haram ya Alawiyya unaotekelezwa na mafundi wa Atabatu Alawiyya tukufu kamati ya ujenzi wa Ataba tukufu.

Ukafuata ujumbe wa wakfu Shia ulio wasilishwa na Shekh Haidari Sahalani, akaeleza mambo yaliyo tokea katika Dini baada ya tukio la Ghadiir, na namna wanafiki walivyo washambulia Ahlulbait (a.s), zaidi akishambuliwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), akazungumza athari ya tukio hilo katika jamii ya watu wa sasa pamoja na mambo ya wazi yanayo onekana.

Ratiba ya hafla ikaendelea kwa kusikiliza ujumbe wa mtafiti wa kiislamu kutoka nchini Misri Dokta Ahmadi Nafisi, akaongea kuhusu utukufu wa siku ya Ghadiir na Ahlulbait (a.s) ambao ni mti unaotoa matunda wakati wote kwa idhini ya Mola wake, kuanzia kiongozi wa waumini (a.s) hadi Imamu Hujjat (a.f), kisha mkuu wa utendaji katika kamati ya ujenzi wa Ataba tukufu Mhandisi Muhammad Dhabihi Karimi akazungumza, hatua za utekelezaji wa mradi wa kuweka dhahabu katika mnara wa kusini mwa malalo.

Mashairi yalikua na nafasi maalum katika ufunguzi wa kongamano hilo, ufunguzi huo ulipambwa na kaswida ya mshairi wa Atabatu Alawiyya Haidari Razaaq Shamrani, hafla ikahitimishwa kwa kuzindua mnara wa kusini wa Haram takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: