Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho ya vitabu yanayo fanyika kwenye kongamano la Ghadiir

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, imeshiriki katika maonyesho ya vitabu yanayo fanyika pembezoni mwa kongamano la Ghadiir linalo simamiwa na Atabatu Alawiyya katika mji mtukufu wa Najafu, maonyesho hayo yamepata mwitikio mkubwa kutoka kwa Ataba za Iraq, Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya, aidha Masjid Kufa na Masjid Sahala pamoja na wakfu Shia na Sunni pia wameshiriki.

Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limesheheni machabisho ya kituo cha Ameed Duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat, na kituo cha kuhuisha turathi pamona na kituo cha masomo ya kimkakati, kimekuja na nakala karibu (300) zinazo tokana na uhakiki pamoja na machapisho ya Ataba tukufu.

Pia tawi lina mausua nyingi, lina mausua ya Shekh Mudhwafar, Alamma Urbadadi pamoja na majarida ya kielimu kutoka katika vituo vilivyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, pamoja na machapisho mengine kama vile jarida la watoto familia na mwanamke.

Fahamu kua kila aliye shiriki katika maonyesho alikua na machapisho yake yatokanayo na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani Ataba ina machapisho ya aina zote, kuanzia Falsafa, Didi, Aqida, Turathi na mambo ya kijamii.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya vitabu ya kitaifa na kimataifa, yanayo lenga kusambaza fikra za uislamu halisi pamoja na kuwapa wasomaji wanacho hitaji katika fani mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: