Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumatano (26 Dhulhijja 1440h) sawa na (28 Agost 2919m) kimehitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa idara ya mazingira ya mkoa wa Karbala yaliyo dumu kwa muda wa siku tatu.
Hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo ilikua na muhadhara wenye anuani isemayo: (Nani wewe?) uliokua unalenga mtu kujua uhalisia wake, kisha washiriki wakapewa nafasi ya kutembea katika kituo cha kibiashara cha Afaaf kwa ajili ya kuwapa fursa ya kuangalia maendeleo ya kiujenzi na kununua mahitaji yao, mwisho kabisa wakaenda kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kufanya ziara.
Siku ya kwanza ilikua na mihadhara miwili, muhadhara wa kwanza ulikua unasema: (Kuwasiliana na watoto) ulieleza hatua muhimu anazoweza kutumia mama ili kukuza uhusiano kati yake na mwanae, na muhadhara mwingine ulikua unasema: (Nguvu ya fikra chanya) ulieleza tofauti ya fikra chanya na hasi, na namna ya kunufaika na fikra chanya.
Siku ya pili ilikua na mihadhara miwili pia, wa kwanza ulikua unasema: (Misingi ya kufaulu uhusiano wa wanandoa), huku muhadhara wa pili ukizungumzia (Tiba lishe kwa tatizo la kuongezeka uzito) ulieleza tatizo la uzito kiafya na namna ya kujiepusha nalo kwa kutumia lishe.
Fahamu kua kituo cha utamaduni wa familia pamoja na kwamba kipo katika mwaka wa pili tangu kianzishwe, kimeleta mabadiliko makubwa kwa wanawake kupitia mihadhara tofauti na ratiba mbalimbali, kinafanya juhudi kubwa kuhakikisha familia zinaishi katika mazingira mazuri na jamii kwa ujumla.
Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia kimejikita katika mambo ya familia na jamii, ofisi zake zipo katika mkoa wa Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Hussein (a.s) ndani ya jengo la kituo cha Swidiqah Twahira (a.s). kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba ifuatayo (07828884555).