Kuandaa mfumo wa kuongeza uzaaji wa kondoo katika kitengo cha ufugaji wa wanyama chini ya shirika la kibiashara Alkafeel

Maoni katika picha
Kikosi cha watalamu wa kitengo cha kilimo na mifugo ya wanyama katika shirika la kibiashara Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza kuandaa mfumo wa kuongeza uzaaji wa kondoo, tunatarajia kushuhudia ongezeko la uzaaji wa kondoo tofauti na misimu iliyo pita.

Rais wa kitengo cha kilimo na ufugaji wa wanyama katika shirika la kibiashara Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Ali Mazál Laaidh amesema kua: “Hakika watalamu tofauti wametoa chanjo za kuwalinda kondoo na maradhi ya kuambukiza pamoja na kuwapa dawa za kuongeza uzaaji sambamba na kuwalinda na wadudu ambao huharibu manyoya yao”.

Akasisitiza kua: “Kazi hiyo imefanywa sambamba na kusafisha zizi zote na kuzitandika kwa vitu maalum ili kuweka mazingura muwafaka katika msimu huu wa miezi ya uzaaji wa kondoo, kutokana na matarajio yetu ya kuongezeka kwa kiwango cha uzaaji kufuatia maandalizi yaliyo fanyika tangu mwanzoni mwa msimu huu”.

Akafafanua kua: “Zimeandaliwa zizi maalim kwa ajili ya kondoo wenye mimba ili iwe rahisi kuwapa chakula maalum kinacho wasaidia kuzaa watoto wenye afya nzuri”.

Kumbuka kua kitengo cha kilimo na ufugaji wa wanyama katika shirika la kibiashara kinatumia njia za kisasa kuongeza uzaai wa kondoo bora zaidi wa aina ya Naimi na Awaasi, na nyama zao huuzwa katika vituo vya Alkafeel vya maozo ya moja kwa moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: