Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, amesema kua amani ya fikra humpa mtu utulivu na humkinga na shirki pia husaidia kupambana na changamoto za amani katika jamii, amesema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye ufunguzi wa kongamano la Naaswiru lisilmi Aamniy wal-mujtamaiy la kwanza, asubuhi ya Alkhamisi (27 Dhulhijja 1440h) sawa na (29 Agost 2019m) linalo simamiwa na kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Akaongeza kua: Atabatu Abbasiyya tukufu imesisitiza umuhimu wa amani ya jamii, ni msingi muhimu wa kupata utulivu wa maisha na ustawi wa jamii, kwa ajili ya yote hayo Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi imekua ikifanya program mbalimbali za kuhubiri amani kupitia vitengo vyake, kama vile kitengo cha habari na utamaduni, malezi na elimu ya juu, maarifa ya kiislamu na kibinadamu na vinginevyo, kwa kuamini kua swala la Amani ni jukumu la kijamii, sio jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama peke yake, bila kusahau amani ya kifikra ndio msingi wa kumlinda mtu na changamoto za kijamii”.
Akabainisha kua: “Leo kitengo cha kulinda nidham kinafanya kongamano la kwanza kwa jina la (Naaswiru lisilmi amniy wal-mujtamaiy) kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii yetu pamoja na kupambana na fikra potofu ambazo huwa na matokeo mabaya, sambamba na kulinda misingi ya jamii njema inayo takiwa kuimarishwa na kudumishwa, Mwenyezi Mungu awawezeshe wasimamiaji wa kongamano hili pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama aidha awape nguvu watu wote wanao shiriki katika vikao vya kitafiti”.