Kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Unapo andama mwezi wa Muharam malaika hukunjua kanzu ya Hussein (a.s) ikiwa imelowa damu, sisi na wanaotupenda huiona kwa moyo sio kwa macho, tukio hulo hulihisi katika hisia zetu na huumiza nafsi zetu…).
Kutokana na maneno hayo hali yetu sawa na Ataba zingine na mazaru tukufu za ndani na nje ya Iraq pamoja na misikiti na Husseiniyya, kila upande wa haram tukufu imetanda huzuni kutokana na msiba huu.
Kitengo cha usimamizi wa Haram tukufu kimefanya kazi ya kuweka mazingira ya huzuni na maombolezo, baada ya kitengo cha ushonaji kumaliza kazi yake ya kushona vitambaa maalum kwa ajili ya maombolezo hayo, wametengeneza mabango, bendera na vitambaa vya kufunga ukutani vinavyo akisi huzuni na majonzi, kitengo kimeanza kazi hii zaidi ya siku sita zilizo pita, na kinatarajia kumaliza kabla ya kupandishwa bendera ya maombolezo ya Husseini.
Mazingira ya huzuni yameenea kila sehemu ndani ya haram tukufu na maeneo yanayo zunguka haram, kuna mapambo yaliyo andikwa aya za Quráni tukufu, mashairi na semi mbalimbali zinazo ashiria majonzi, pamoja na bendera nyeusi, tutakupeni habari kamili baada ya kukamilika kazi hii na kubadilisha bendera ya Kubba takatifu.