Watu wa Karbala na mawakibu zao wanajiandaa kupokea msimu wa huzuni, na kitengo cha maadhimisho chaweka utaratibu wa mawakibu za waombolezaji

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia mwezi wa huzuni tunaokumbuka kuuwawa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake, watu wa Karbala wameanza kuandaa mazingira ya kuomboleza msiba huu katika kila sekta, vitambaa vyeusi vimeanza kuenea kila kona ya mji kidogo kidogo, mawakibu nyingi na vikundi vya Husseiniyya vina andaa sehemu zao kwa kujenga mabanda na mahema na kuweka vifaa watakavyo tumia kutoa huduma kwa mazuwaru.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni-mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Watu wa Karbala wameanza kujiandaa kuupokea mwezi wa huzuni, mwezi mtukufu wa Muharam, maandalizi haya ni desturi ya watu wa Karbala baada ya Idul-Ghadiir, wanaimarisha ulinzi na kufanya maandalizi mbalimbali ya kuomboleza siku za msiba”.

Akaongeza kua: “Maandalizi haya yalianza kwa kufanya makongamano mbalimbali yaliyo husisha viongozi wa mawakibu na vikundi vya waombolezaji, ukiwemo mkutano ulio wakutanisha viongozi wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya pamoja na viongozi wa Ataba mbili tukufu, kikoa hicho kilijadili mambo mengi na kukubaliana vipengele vitakavyo saidia kufanya maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) katika mazingira mazuri”.

Barabara kubwa na ndogo za mji wa Karbala hasa katika maeneo yanayo zunguka malalo mawitu tukufu, zimejaa watu wanaojenga mabanda na mahema ya kufanya vikao vya kuomboleza na kutoa huduma mbalimbali, miongoni mwa mambo waliyo zewea kufanya watu wa Karbala ni kujenga mabanda ya Husseiniyya kwa ajili ya kusaidia mazuwaru watukufu, jambo hilo ni urithi wa watu wa mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: