Mafundi wa ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kushona bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) itakayo pandishwa Muharam mosi (1441h) baada ya swala ya Maghribi na Isha kama tangazo la kuanza kwa mwezi wa huzuni, itapandishwa sambamba na bendera ya kubba la ndugu yake Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika hafla maalumu ya kuomboleza ambayo imekua ikifanywa kila mwaka tangu mwaka (2005m).
Kiongozi wa kitengo cha ushonaji Ustadh Abdu-Zahara Daudi Salmaan ametuambia wasifu wa bendera hiyo kua: “Kazi ya kushona bendera hiyo hupita hatua nyingi, kuanza kuchagua kitambaa, ambapo huchaguliwa kitambaa bora zaidi na imara, kinacho weza kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa na kisicho pauka, kisha huchukuliwa vipimo maalum, halafu huanza kazi ya ushonaji, miongoni mwa sifa muhimu za bendera hiyo:
- - Imeshonywa na kudarizwa vizuri kwa kitambaa bora na imara.
- - Inaupana wa mita tatu na nusu (mt3.5) na urefu wa mita mbili na nusu (mt2.5).
- - Inapande mbili, kila upande umeandikwa neno lisemalo: (Ewe mnyweshaji wenye kiu Karbala) maneno hayo yanahusu mwezi wa Muharam na Sarar, yameandikwa kwa hati ya Thuluth na mchoraji mahiri bwana Farasi Asadiy.
- - Maandishi yana ukubwa wa mita mbili na senti mita ishirini (mt2. sm20) katika eneo lenye ukubwa wa mita mbili na nusu (mt2.5) katika eneo lote la bendera na inarangi nyekundi.
- - Inauzito wa kilo mbili na nusu takriban (2.5).