Kongamano la Multaqal-Qamaru linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu limekamilisha awamu ya kumi na nne kwa walimu wa Bagdad.
Kongamano hilo linalenga watu wa tabaka tofauti katika jamii, kwa ajili ya kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, na kujibu changamoto hizo kwa kutumia elimu, wala sio nguvu na chuki vitu ambavyo huwa na matokeo mabaya katika jamii.
Mhadhiri wa kongamano hilo Ustadh Farasi Shimri amesema kua: “Kongamano lilichukua siku tatu mfululizo, washiriki wamepewa mada zinazo husu utamaduni, aqida na dini, zinazo wawezesha kuathiri jamii, ukizingatia kua wanafanya kazi na tabaka muhimu la watu ambao ni wanafunzi wa sekondari”.
Akaongeza kua: “Ratiba ya mihadhara ilihusisha mada ya kujibu shubuha (utata) iliyo tolewa na Shekh Harith Dahi, na mada ya uhalisi wa Dini ilitolewa na Shekh Hassan Jawadi, hali kadhalika kulikua na mada ya utambuzi wa hisia iliyo tolewa na Shekh Ali Saidi pamoja na mada kuhusu njia za ufundishaji za kisasa”.
Washiriki wameushukuru sana uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu bila kumsahau kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kutokana na mada nzuri walizo fundishwa zinazo wawezesha kubadilisha mitazamo na kuendana na jamii, kongamano likafungwa kwa kugawa zawadi na vyeti vya ushiriki.