Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru wanaokuja kushiriki katika tukio la kubadilisha bendera za malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo kilele cha shughuli hiyo ni jioni ya leo (29 Dhulhijja 1440h) sawa na (31 Agost 2019m), tukio hilo adhim litafanywa baada ya swala ya Magharibi na Isha, hii ni desturi ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbaiti kwa miaka mingi sasa, kubadilishwa bendera hizo huchukuliwa kama tangazo la kuanza kwa msimu wa huzuni.
Wamekusanyika mazuwaru wengi mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hasa mbele ya mlango wa Kibla, kwani uwanja wa mbele ya mlango huo ndipo itakapo fanyika shughuli hiyo, na kukumbuka yaliyo tokea kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kablba ya zaidi ya miaka (1400), kundi hilo la mazuwaru linashiriki hatua zote za ubadilishaji wa bendera na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali ibada zao kwa baraka za waliosimama mbele ya malalo yake tukufu, na awajalie kua miongoni mwa wanaofuata mwenendo wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Fahamu kua miongoni mwa maandalizi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni kuandaa sehemu maalum ya kufanyia tukio hili nayo ni uwanja wa mbele ya mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika eneo hilo ndio kuna jukwaa kwa ajili ya kupandisha bendera nyeusi itakayo pandishwa sambamba na tukio la kubadilishwa bendera ya kubba tukufu, shughuli hiyo itaambatana na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kupata ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na kukabidhi bendera ya msiba kwa moja ya mikoa ya Iraq, shuguli ya kupandisha bendera nyeusi mahala pa bendera nyekundu itafanyika pembeni ya jukwaa, halafu itabadilishwa bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhitimisha kwa kaswida za kuomboleza.
Kumbuka kua jambo hili limekua likifanyika kila mwaka tangu mwaka (2004), tukio hilo ni sawa na tangazo la kuanza kwa msimu wa huzuni, na huzuni huanzia Karbala tukufu mji mkuu wa maombolezo ya Husseiniyya.