Tunabaki katika ahadi na kuhuisha utajo wako: Mawakibu za kuomboleza Ashura zimeanza maombolezo

Maoni katika picha
Mawakibu za kuomboleza Ashura katika siku kumi za kwanza kwa watu wa Karbala, na huu ni utamaduni wa miaka mingi ambapo huwa kuna maukibu za waombolezaji za (zanjiil), kutoka kila sehemu ya makao makuu ya maadhimisho ya Husseiniyya Karbala ya shahada na undugu, wakiwa wamebeba bendera nyeusi huku wanapiga vifua vyao na kuonyesha huzuni kwa kufiwa na mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein bun Ali (a.s) na watu wa nyumbani kwake.

Matembezi na uingiaji wa mawakibu unafanyika kwa kufuata ratiba iliyo pangwa na kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya, na kwa usimamizi wa watumishi wake ili kuzuwia muingiliano au kutatiza harakati za mazuwaru.

Kumbuka kua mawakibu za waombolezaji (zanjiil au matam) huanza maombolezo yao tangu siku ya kwanza ya muharam asubuhi na jioni, kwa kufanya matembezi katika barabara zinazo elekea kwenye Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na matembezi yao huishia katika kaburi la Abu Abdillahi Hussein (a.s) baada ya kupita katika kaburi la ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: