Kitengo cha utumishi kimemaliza kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni nje ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Miongoni mwa kazi za kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye msimu wa huzuni za Ashura katika kukumbuka kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s), ni kuweka mapambo meusi nje ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo zunguka haram, mapambo ambayo huashiria huzuni na maombolezo kwa Ataba na mazuwaru wake.

Mkuu wa kazi hiyo bwana Riyadh Khadhiir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika kila msimu wa kuomboleza hususan mwezi wa Muharam na Safar huwa tunaweka mapambo meusi na mabango yanayo ashiria maombolezo ya Husseiniyya ya Ashura, kazi hiyo hutanguliwa na kazi ya kubaini maeneo ya kuweka mapambo na mabango hayo, kisha huchukua vipimo na kuandaa mapambo yanayo hitajika, ambayo huwekwa sehemu tofauti, na kuna sehemu za kudumu ambazo huwekwa mabambo hayo kama vile:

  • - Mlango wa Kibla na wa Imamu Hassan (a.s).
  • - Kwenye maandishi ya Quráni yanayo zunguka haram tukufu kwa nje.
  • - Nguzo na kuta za nje.
  • - Uzio wa nje unao zunguka Ataba tukufu upande wa uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
  • - Sehemu na majengo yaliyo karibu na Ataba tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: