Ilitokea siku kama ya leo mwezi pili Muharam mwaka wa 61 Hijiriyya: Kuwasili msafara wa Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala…

Maoni katika picha
Imamu Hussein (a.s) alitoka Maka hadi katika ardhi ya Karbala, alikua akikumbuka kisa cha Nabii Yahya (a.s) na anasema: (Miongoni mwa uwovu wa duniani mbele ya Mwenyezi Mungu ni kutolewa zawadi kwa kichwa cha Yahya mtoto wa Zakariya kwa Malaya miongoni mwa Malaya wa wana wa Israeel) kwa nini? Ili awakumbushe walio pamoja naye kua harakati yake sio kwa ajili ya kutafuta madaraka, au kupata umashuhuri, bali ni kwa ajili ya kutafuta akhera kwa sababu dunia imesha haribika, kwa hiyo anakwenda kufuata jambo ambalo litasababisha auwawe kama alivyo uwawa Yahya mtoto wa Zakariya.

Anatoka Maka kwenda Iraq akiwa anajua mambo yatakayo mtokea, Imamu Hussein (a.s) alikua anajua kua atauwawa, lengo la safari yake halikua Iraq japokua ndio sehemu liliko fanyika tukio, lengo lake ni kwenda akhera, na kubakiza misingi ya heshima na utukufu.

Ndio maana katika safari hiyo Imamu Hussein (a.s) alikua anarudia rudia kusema: (Hayo ndio makaazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasio taka kujitukuza duniani wala usifadi. Na mwisho mwema ni wa wachamungu) kwa ajili ya kuwakumbusha watu alio nao malengo ya safari hiyo.

Msafara wa Imamu Hussein (a.s) ulikua na vituo vingi, kituo cha mwisho kikawa katika ardhi ya Karbala, alifika sehemu hiyo siku kama ya leo, mwezi pili Muharam mwaka wa 61 Hijiriyya, Imamu (a.s) alikua anauliza kanakwamba anatafuta ardhi ya Karbala, alisema: (Ardhi hii inaitwaje)? akaambiwa: Inaitwa Twafu. Akauliza tena: (Je! Inajina tofauti na hilo)? akaambiwa: Inaitwa Karbala. Akasema (a.s): (Ewe Mola najilinda kwako na shida na balaa).

Kisha (a.s) akasema: (Hapa tutapata shida na balaa, shukeni, hapa ndio mwisho wa safari yetu sehemu itakapo mwagika damu yetu, na ndio sehemu ya kaburi zetu, hivi ndio alivyo nihadithia babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu –s.a.w.w-), siku ya Alkhamisi ndio siku aliyo wasili Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala na akafunga hema zake na akaanza kuandaa siraha huki anasoma beti zifuatazo:

Ewe dahari koma kwa mpenzi *** mara ngapi umechomoza.

Kwa rafiki au ukatafuta kifo *** na dahari haitosheki kwa mbadala.

Hakika amri ni ya Jaliil *** kila aliye hai atapita katika njia.

Bibi Zainabu (a.s) alipo sikia beti hizo, akasema: (Ewe kaka yangu haya ni maneno ya mtu mwenye yakini ya kuuwawa)! Akasema (a.s): (Ndio ewe dada yangu). Bibi Zainabu akasema: (Msiba ulioje, akaanza kumlilia Hussein).

Hema za msafara wa Imamu Hussein (a.s) zilifungwa sehemu takatifu, athari ya sehemu hiyo bado ipo hadi leo katika ardhi ya Karbala, ilikua mbali na maji na imezungukwa na miinuko kadhaa, lilifungwa hema lake na hema la watu wa nyumbani kwake (a.s) kisha yakafungwa mahema ya wanafamilia wake halafu yakafungwa mahema ya wafuasi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: