Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu: Yahitimisha semina ya usomaji wa Quráni na Tajwidi

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za kufundisha utamaduni wa Quráni, Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Naafu chini ya Atabatu Abbasiyya imehitimisha semina ya hukumu za usomaji wa Quráni na tajwidi, kwa kuwapa mtihani wanasemina.

Mtihani wamefanya kwa muda wa siku mbili mfululizo, siku ya kwanza wamefanya mtihani wa somo la Tajwidi na siku ya pili wakafanya mtihani wa nadhariyya katika somo hilo hilo.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inaendelea na miradi ya Quráni mwaka mzima, ambayo huwalenga watu wenye umri na elimu tofauti, hufanya miradi mbalimbali ya Quráni tukufu, na huwapa kipaombele vijana wenye vipaji kwa kuendeleza vipaji vyao vya kuhifadhi na usomaji sambamba na kuwapa kila wanacho hitaji, pia Maahadi hushirikiana na taasisi zingine za Quráni kwa ajili ya kubadilishana uzowefu na hushiriki katika mashindano na makongamano ndani na nje ya Iraq, pamoja na kuandaa mubalighina katika sekta ya Quráni kwa kutoa mafunzo maalum ya uwalimu wa Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: