Ilitokea siku kama ya leo mwezi tatu Muharam mwaka 61h: Kuwasili kwa jeshi la Omari bun Saadi katia ardhi ya Karbala kwa ajili ya kupigana na Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Ubaidullahi bun Ziyadi (laana iwe juu yake) alituma jeshi katika ardhi ya Karbala, miongoni mwa makamanda wakuu aliowatuma kwenda kupigana na Imamu Hussein (a.s) ni Omari bun Saadi, akamuahidi kama akiweza kumuua Hussein (a.s) atampa ugavana katika jimbo la Rai, Omari bun Saadi akachagua starehe za dunia, akaenda na jeshi la wapiganaji elfu nne, akaweka kambi karibu na hema za Hussein (a.s) aliyekua amefika hapo siku moja kabla yake.

Idadi ya wanajeshi:

Ubaidullahi bun Ziyadi –gavana wa Kufa- alituma wapiganaji elfu thelathini, na inasemekana walikua elfu arubaini, wote walikua chini ya Omari bun Saadi katika ardhi ya Karbala, kwa ajili ya kupigana na Imamu Hussein (a.s), akamuahidi kama akiweza kumuua Imamu Hussein (a.s) atampa ugavana wa jimbo la Rai, jeshi hilo lilifika Karbala mwezi tatu Muharam mwaka 61 Hijiriyya.

Kukutana kwa Omari bun Saadi na Imamu Hussein (a.s):

Omari bun Saadi alikutana na Imamu Hussein (a.s), akamuuliza sababu za kuja kwake katika mji wa Kufa, Imamu akamwambia: (Watu wa mji huo wameniandikia barua za kuniomba nije, kama hamtaki naweza kwenda sehemu nyingine).

Barua ya Omari bun Saadi kwa ibun Ziyadi:

Omari bun Saadi akamwandikia barua ibun Ziyadi, akimwambia maoni yake baada ya kuongea na Imamu Hussein na kumuomba wampe ruhusa ya kurudi na wasipigane naye.

Barua ya ibun Ziyadi kwa Omari bun Saadi:

Ibun Ziyadi akajibu barua hiyo kupitia barua iliyo andikwa na Shimri bun Dhiijaushen (laana iwe juu yake) akamwambia shimri kua: Amwambie Hussein na watu wake wale kiapo cha utii, wakikubali awalete kwangu kwa amani na wakikataa awauwe, Omari akitekeleza agizo hili kua chini yake na umtii na kama akikataa wewe utakua kamanda mkuu utakae ongoza vita na ukate kichwa chake na uniletee, miongoni mwa maneno yaliyo kua katika barua hiyo ni: (Mimi sikukutuma kwa Hussein ukaongee nae, wala kumpa amani na kumuacha hai, au kumuombea msamaha, angalia! Kama Hussein na watu wake watakula kiapo cha utii kwangu, walete kwa amani, wakikataa watese, wauwe na usulubu maiti zao, hakika wanastahiki kufanyiwa hivyo, baada ya Kuuwawa Hussein amrisha farasi zikanyage kanyage kifua chake na mgongo wake, ukitekeleza amri yetu tutakulipa kwa usikivu na utiifu, na ukikataa achia madaraka na Shimri Dhijaushen ataongoza jeshi hakika yeye tumesha mpa amri yetu, wasalam).

Msimamo wa Omari bun Saadi:

Omari alipokea barua na akaisoma, akawa anapigana na nafsi yake baina ya kupigana na Imamu Hussein (a.s) na kumuua, ili apate uongozi na heshima kwa watu wake na apate dhambi na laana, nafsi yake ikamtuma achague uongozi na mali, akakubali kuongaza vita dhidi ya Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake chini ya usaidizi wa Shimri bun Dhijaushen.

Omari bun Saadi akamtaka Imamu Hussein (a.s) ale kiapo cha utii, akikataa atamzuwia kuchota mati (katika mto Furaat), Imamu (a.s) pamoja na ukubwa wa jeshi la Omari na uchache wa wanajeshi wake lakini alikataa kula kiapo cha utii, akasema: (Tambueni hakika muovu mtoto wa muovu ametupa kuchagua baina ya mambo mawili, baina ya kupigana au udhalili, uwe mbali nasi udhalili, Mwenyezi Mungu hataki hilo kwetu na Mtume wake na waumini…).

  • - Raudhat Waaidhiin 1182.



#Ashura_minhaaj
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: