Aliwaambia Hussein… Ewe Habibu, ulikua unasoma Quráni nzima kwa usiku mmoja

Maoni katika picha
Hakutoka bwana wa mashidi (a.s) ispokua kwa ajili ya kunusuru kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, baada ya kupuuzwa na matwaghuti wa zama zake na wakaikhalifu waziwazi, Imamu Hussein (a.s) alikua mchamungu, msomaji mkubwa wa kitabu kitukufu na mwenye kuzitafakari aya zake takatifu, aliyo sema baba wa watu huru kwa mfuasi wake Habibu bun Mudhwahir Al-Asadiy (r.a) wakati wa kifo chake katika vita ya Twafu ulikua ni uthibitisho wa hilo.

(Unautukufu mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ewe Habibu, ulikua unasoma Quráni nzima kwa usiku mmoja) Abu Abdillahi Hussein (a.s) alimuaga rafiki yake Habibu bun Mudhwahir Asadiy kwa maneno hayo, aliyekua anajulikana kwa utukufu, uongofu, uchamungu, ushujaa na msimamo, aliuwawa kwa ajili ya kupigania haki na kumnusuru Imamu wa zama zake akaacha jina lake katika kurasa za makamanda wa kiislamu.

Hakua Hussein ispokua ni msomaji wa Quráni tukufu na mwenye kufanyia kazi mafundisho yake, Habibu buna Mudhwahir Al-Asadiy (r.a) aliuwawa kwa ajili ya kumnusuru bwana wa mashahidi (a.s) na kuendeleza mwenendo wa Muhammad na Aali Muhammad (a.s).

#Ashura_minhaaj
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: