Hussein alimuambia… wewe ni Huru kama mama yako alivyo kwita, wewe ni Huru duniani na akhera

Maoni katika picha
Njia ya Imamu Hussein (a.s) ilikua njia ya uhuru na kupinga dhulma, hadi jambo hilo likawa ndio kauli mbiu inayo somwa na wafuasi wa madrasa ya Ahlulbait (a.s), katika kupambana kwao na kila muovu mwenye kuwafanyia uwadui katika Dini na ardhi zao, haikusadifu tu kuuwawa kishahidi mbele ya baba wa watu huru (Abul-Ahraar) (a.s) kwa swahaba mtukufu aitwae Huru, mtu ambaye jina lake liliendana na sifa yake, ikawa jina limeendana na kitendo.

Huru bun Yazidi Ariyahi (r.a) alikua katika upotovu, akapata uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akajiunga na Imamu Hussein (a.s), akatoka katika jeshi la upotovu na kuingia katika jeshi la uongofu, akashikamana sana na Imamu (a.s) baada ya kusamehewa, akaruhusiwa kupigana kwa ajili ya kuwalinda watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na baada ya kuuwawa kwake Imamu (a.s) akasema maneno mashuhuri yafuatayo: (Wewe ni Huru kama ulivyo itwa na mama yako, na wewe uko huru duniani na akhera).

Tukio la Twafu litaendelea kua somo kwa wanadamu wa kila zama, tukio hilo linamafundisho mengi sana ambayo ni mwongozo kwa kila anayefuata mwenendo wa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: