Miongoni mwa harakati za kila mwaka wanazo fanya katika kuwahudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Jumuiyya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu inatekeleza ratiba ya tatu iitwayo (Labbaika ewe Hussein), ratiba hiyo inahusisha kazi tofauti, ikiwa ni pamoja na kugawa maji ya kunywa kwa mazuwaru kama sehemu ya kumuenzi mnyweshaji maji mtukufu Abulfadhil Abbasi (a.s), vijana wa Skaut wamewekwa katika barabara zinazo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kulinda uzuri wa barabara na kudumisha usafi kama sehemu ya kufanyia kazi hadithi ya Mtume (s.a.w.w) isemayo (Jisafisheni hakika hatoingia peponi ispokua msafi).
Katika ratiba hiyo vijana wa Skaut wanawapulizia manukato mazuwaru waliopo karibu na haram mbili tukufu.
Fahamu kua jumuiya ya Skaut Alkafeel katika idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni huendelea kutekeleza ratiba za Skaut kwa wanafunzi wa shule ndani ya mwaka mzima.