Mkutano na wizara ya vijana na michezo wajadili mikakati na miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Maitham Zaidi ametembelea makao makuu ya wizara ya vijana na michezo katika mji mkuu wa Bagdad, kwa lengo la kujadili mikakati na miradi inayo kusudia kunufaisha vijana.

Amefanya mazungumzo na mkuu wa mikakati na ufuatiliaji katika wizara hiyo Dokta Akram Shawili kuhusu nyanja za kushirikiana katika kuhudumia vijana, na kutoa kipaombele kwa tabaka la vijana kama Atabatu Abbasiyya inavyo fanya kwa tabaka hilo.

Ustadh Maitham Zaidi akauambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Mara hii Atabatu Abbasiyya tukufu imetaka kuweka mikakati ya pamoja na wizara ya vijana na michezo katika baadhi ya harakati zinazo husu vijana, ukizingatia kua vijana ndio viongozi wa baadae na ndio hazina kubwa ya taifa, wao ndio nguvu kazi kuu inayo tegemewa kurekebisha hali ya taifa”.

Akaongeza kua: “Mazingira chanya yameonekana katika kikao hiki na kitazaa utekelezaji utakao tangazwa hapo baadae”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: